Kuendelea kwa upanuzi wa Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f).

Maoni katika picha
Mafundi na wahandisi wanaofanya kazi katika mradi wa kupanua Maqaam ya Imamu Mahadi (a.s) wanaendelea na kazi baada ya kusimama katika kipindi cha msimu wa ziara ya Arubaini, wamesha piga hatua kubwa na picha imeanza kuonekana siku baada ya siku.

Kwa mujibu wa maelezo ya kitengo cha uhandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ambao ndio wasimamizi wakuu wa mradi huu, kazi inayo endelea hivi sasa ni kuweka maraya kwenye dari na kwenye kuta za kumbi, (upande wa sehemu ya wanawake unaukubwa wa mita za mraba (490), na sehemu ya ukumbi wa wanaume inaukubwa wa mita za mraba (310), sehemu ya watumushi wa Maqaam inaukubwa wa mita za mraba (150), sehemu iliyo baki katika uwanja ni ya huduma ya vyoo), sambamba na kuendelea kuweka Kashi Karbalai sehemu ya mbele na nyuma ya Maqaam, inayo husisha mlango mkuu wa Maqaam na sehemu ya mlango wa zamani kwa nje na kufuatiwa na pambo lenye ukubwa wa mita nne, pembezoni mwake kuna nguzo nyingine zitakazo wekwa Kashi Karbail pia, katika kazi hii wametumia vyuma nayo ni nyongeza mpya katika mradi huu.

Tumemaliza kuweka sehemu kubwa ya mambo muhimu katika mradi, kama vile taa, milio ya tahadhari, zima moto, mawasiliano, ulinzi na mengineyo, aidha tumemaliza kujenga na kusakafia mnara wa saa uliopo upande wa mbele.

Kumbuka kua Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseiniyya wa sasa, unapo ingia Karbala kwa kutumia barabara inayo elekea kwenye Maqaam ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) ambayo ni mazaru mashuhuri, Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya matengenezo na upanuzi wa Maqaam hiyo kwa kuanzia kwenye kubba hadi kwenye kumbi za haram na sehemu zingine, kwa kuwa sehemu ilipo Maqaam hauwezi kufanya upanuzi pande zake tatu, imepidi upanuzi ufanywe upande wa mto wa Husseiniyya ambao ni upande wa magharibi, kwa kutumia nguzo za zege na kujenga kama daraja ili kutozuwia maji au kubadilisha njia yake, eneo lililo ongezwa linakadiriwa kufika mita za mraba (1200) na unaweza kufika katika Maqaam kwa kutumia milango maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: