Kujadili namna ya kuboresha ushirikiano na kufanya kazi pamoja: Wanafunzi wa hauza kutoka Najafu wametembelea ofisi ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu.

Maoni katika picha
Wanafunzi wa hauza kutoka Najafu wametembelea ofisi ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuangalia harakati za kitengo hicho na namna ya kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja baina ya pande mbili katika kuhakiki turathi za nakala kale.

Ugeni umepokelewa na rais wa kitengo Shekh Ammaar Hilali, baada ya kuwakaribisha wageni akawaelezea kuhusu miradi ya uhakiki na faharasi inayo fanywa na kitengo hicho, sambamba na majarida semina na vitabu wanavyo andika kuhusu utamaduni na turathi, akaonyesha kua wako tayali kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya kulinda turathi za Ahlulbait (a.s), akasisitiza umuhimu wa kuunganisha nguvu na kuendelea kutembeleana kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya turathi na uhakiki wa nakala kale.

Wageni wamesifu kazi kubwa inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika kulinda na kutunza turathi za kiislamu, kwa kuandika vitabu vinavyo husu historia ya turathi za Ahlulbait (a.s), na kufanya mikutano, nadwa, maonyesho ya turathi na harakati zingine ndani na nje ya Karbala, wakaonyesha utayari wao wa kushirikiana katika kila kitu kinacho husu kulinda na kutunza turathi za Ahlulbait (a.s), mwishoni mwa mazungumzo yao rais wa kitengo akawazawadia wageni sehemu ya machapisho ya kitengo hicho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: