Mgahawa wa Atabtu Abbasiyya tukufu unaendelea kuhudumia watu wanaoandamana kwa amani.

Maoni katika picha
Miongoni mwa jitihada za kuunga mkono watu wanaofanya maandamano ya amani na kudai haki zao kisheria walizo pewa na katiba na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mgahawa wake bado inaendelea kugawa maelfu ya sahani za chakula kwa waandamanaji na kutoa huduma za matibabu.

Mgahawa umeitikia sehemu ya maombi ya waandamanaji walio weka kambi katika uwanja wa Tarbiyya hapa mkoani Karbala, kwa kugawa chakula mara mbili kila siku pamoja na mahitaji mengine muhimu, sambamba na kugawa maji na juisi, chakula hupelekwa kwa gari maalum na kupewa waandamanaji moja kwa moja au kuwekwa kwenye mahema maalum ya kugawia chakula.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma mbalimbali kwa waandamanaji kama ishara ya kuwaunga mkono, miongoni mwa huduma hizo ni:

  • - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula kupitia mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kuwatumia kwa gari maalum.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji safi ya kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa nyakati tofauti.
  • - Kufanya usafi katika maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji kwa kutumia gari maalum za usafi.
  • - Kufungua vituo maalum vya kugawa maji kwa waandamanaji.
  • - Kutoa matibabu bure kwa waandamanaji na askari wanaopata matatizo ya afya katika hospitali ya rufaa Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: