Kazi hiyo ilikua na hatua mbalimbali, miongoni wa hatua hizo ni:
- - Kubadilisha sehemu ya nje iliyokua imefunikwa kwa kuweka miamvuli mipya.
- - Kuunganisha vyuma vyenye mataili kwa ajili ya kuweka mwamvuli juu yake.
- - Kubadilisha miamvuli iliyo haribika na kuweka mipya.
- - Kupaka rangi.
Kumbuka kua miamvuli hii inaukubwa wa (2m36) imetengenezwa Uturuki na inaubora wa hali ya juu.
Kitambaa cha mwamvuli kimetengenezwa kwa (Teflon) kinauwezo mkubwa wa kuvumilia mionzi ya jua na mabadiliko ya hewa, kila mwamvuli unaukubwa wa (mt 6x6) na urefu wa (mt 3.5).
Miamvuli hii inamuda maalum wa kuifungua na kuifunga kutokana na mazingira ya hali ya hewa, wanaofanya kazi hiyo ni watu waliobobea katika shughuli hiyo kutoka kitengo cha utumishi, vitambaa vya miamvuli vinapo chafuka hufunguliwa na kwenda kuoshwa kwenye kituo cha Ataba tukufu kisha hurudishwa na kufungwa upya.