Kwa picha: Mradi wa Waahatu Zaairu unaendelea.

Maoni katika picha
Utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyoo (Waahatu Zaairu) unaofanywa chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu uliopo upande wa mlango wa Bagdad kama unaelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ufadhili wa muhisani unaendelea, utendaji umefika kiwango kizuri, unatarajiwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa.

Ukubwa wa eneo la mradi ni mita za mraba (1500) patakua matundi ya vyoo (200) upande wa wanaume na wanawake katika tabaka la chini, huku tabaka la juu likipandwa majani na kuwekwa njia za maji katika eneo la ukubwa wa mita za mraba (656), kwa ajili ya kuweka mandhari nzuri, pia kuna sehemu maalumu za watu wenye ulemavu, tayali mradi umesha wekewa kila kitu kinacho hitajika, kuna pambu za maji, hita, viyoyozi, mahodhi ya maji, vyumba vya ukaguzi, ofisi na stoo, pamoja na mtambo wa kisasa wa kutoa hewa chafu na kuingiza hewa safi, pia kuna sehemu ya kutawadhia na sehemu ya maji wa kunywa, pia mfumo wa umeme na taa umesha kamilika pamoja na mfumo wa kuzuwia sauti.

Kumbuka kua mradi huu unafanywa kwa ajili ya kuhudumia watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pia ni muendelezo wa miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, mradi huu unajengwa na shirika la ujenzi Twabaaq chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi na kwa ufadhili wa muhisani, katika eneo ambalo halitatizi upanuzi wowote utakao fanywa na Ataba siku za mbele.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: