Sauti wa raia: Haya ndio yaliyo semwa na Marjaa Dini mkuu tarehe (3/6/2011m).

Maoni katika picha
Thamani ya kila kiongozi inatokana na mambo anayo lifanyia taifa, sio anayo fanyiwa na taifa, mtu mwema ni yule anayekiri udhaifu wake na kukubali kujiuzuru wadhifa wake.

Hii ni moja ya nukta iliyo zungumzwa na Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya Ijumaa tarehe (30 Jamadal-Aakhar 1432h) sawa na (3/6/2011), chini ya uimamu wa muwakilishi wake Sayyid Ahmadi Swafi.

Katika khutuba hiyo alizungumza nukta kadhaa muhimu, miongoni mwa nukta hizo ni:

  • Lazima kiongozi awahudumie wananchi na taifa kwa uwezo wake wote, hakika thamani ya kiongozi inatokana na mambo anayolifanyia taifa sio anayo fanyiwa na taifa.
  • Kiongozi anatakiwa aingie kazini akiwa anafahamu majukumu yake, anatakiwa atambue kua uongozi sio tunu ya pesa bali ni kazi na mtihani, anaweza kufaulu au kufeli, ameitwa kiongozi kwa sababu kuna kazi anatakiwa awajibike kuzifanya.
  • Marjaa akauliza –wakati huo-: Je kiongozi hufidia saa alizo chelewa kazini? Je hujiuliza kuhusu pesa anazo pewa mwisho wa mwezi kua kuna pesa asiyo stahiki?! Kiongozi akijiuliza mambo hayo atapendwa na wananchi na atatekeleza wajibu wake.
  • Wanasiasa ndio wanao ongoza taifa, wanawajibika kutatua chamgamoto za kisiasa, kiuchumi, kijamii na zinginezo, (akauliza kwa mshangao!!), yupi bora, viongozi wa chama fulani kupambana kutatua changamoto au kuzusha fitina na kuongeza mfarakano??!, kwa nini vyama vya kisiasa visikubali kumaliza matatizo kwa kutumia wasomi?!!! Kwa nini daima wanatofautina wala hakuna makubalino ya kumaliza tatizo? Jukumu la kiongozi sikutatua changamoto na kumaliza fitina?!!
  • Alizungumzia umuhimu wa kutatua changamoto za taifa, akafafanua kua: “Mtu bora ni yule anayekiri udhaifu wake na kukubali kujiuzulu”.

Alikua akisema haya kwa miaka mingi, kwa masikitiko makubwa hakuna mwanasiasa aliye yafania kazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: