Mwezi kumi na saba Rabiul-Awwali ndio siku aliyo zaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) alizaliwa alfajiri ya siku ya Ijumaa katika mwaka wa tembo, siku ambayo (watu) walikuja na tembo kubomoa Alkaaba tukufu, Mwenyezi Mungu akawaangamiza kwa mawe yaliyotoka katika moto wa Sijjiil.
Twabari amesema kua Mtume (s.a.w.w) alizaliwa mwaka wa arubaini na mbili wa mfalme Anushirwani, kauli hiyo ni sawa, kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Nilizaliwa zama za mfalme muadilifu Anusharwani bun Qabaad aliye wauwa mazandiki).
Alizaliwa ndani ya nyumba katika mji mtukufu wa Maka, kisha Mtume (s.a.w.w) akakabidhiwa kwa Aqiil bun Abu Twalib.
Amina binti Wahabi mama wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) anasema: Alipozaliwa Muhammad (s.a.w.w) alianguka chini (alisujudu), kisha akainua kichwa chake na kuangalia juu, ikatoka nuru iliyo angazia kila kitu, nikasikia sauti ikisema: Hakika umezaa mbora wa watu, mwite Muhammad. Abdulmutwalib akaja kumuangalia akiwa amesha pata ujumbe kutoka kwa mama yake (Mtume) akamuweka miguuni kwake na akasema:
Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye amenipa *** kijana huyu mzuri wa pekee.
Ni mbora wa watoto wote.
Mtume (s.a.w.w) alizaliwa akiwa yatima, baba yake Abdullah bun Abdulmutwalib alifariki wakati akirudi kutoka Sham kupeleka biashara ya baba yake Abdulmutwalib, akaugua na kufariki huku mke wake bi Amina akiwa na mimba ya Muhammad (s.a.w.w), akazikwa kwenye nyumba ya Naabigha katika mji wa Madina.
Abdulmutwalib babu wa Mtume (s.a.w.w) alipo pata taarifa ya kuzaliwa kwa Mtume, alifurahi sana, akaingia kwa bi Amina (r.a) na akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kusema:
Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye amenipa *** kijana huyu mzuri wa pekee.
Ni mbora wa watoto wote namlinda kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.
Hadi nimuone akiwa mkubwa *** namlinda kutokana na shari za waovu.
Namlinda na mahasidi na wenye kijicho.
Imepokewa kutoka kwa Ibun Masoudi anasema: Anasema mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kumuambia Ali bun Abu Twalib (a.s): (Wakati Mwenyezi Mungu alipo muumba Adam na kumpulizia roho, na akasujudiwa na malaika kisha akamuweka peponi yeye pamoja na mke wake bi Hawa, aliangalia juu akaona mistari mitano ya maandishi, Adam akasema: Ewe Mola hawa ni wakina nani? Mwenyezi Mungu akamuambia: Hawa ndio ambao mja wangu akiniomba kwa utukufu wao nampa, Adam akasema: Ewe Mola wanaitwa wakina nani? Akasema: wa kwanza: Mimi ni Mahmuud na yeye ni Muhammad, wa pili: mimi ni Aali mkuu na yeye ni Ali, wa tatu: mimi ni Faatwiru na yeye ni Faatuma, wa nne: mimi ni Muhsin na yeye ni Hassan, wa tano: mimi ni mwenye Ihsaan na yeye ni Hussein, wote wanamhimidi Mwenyezi Mungu mtukufu).
Miongoni mwa majina yake (s.a.w.w) ndani ya Quráni tukufu ni: Khaatamu Nnabiyyiin, Ummiy, Muzammil, Mudathir, Nadhiir, Mubiin, Kariim, Nuur, Ni’mah, Rahmah, Abdu, Rauuf, Rahiim, Shaahid, Mubashir, Nadhiir, Daai.
Masdar: Biharul-Anwaar.