Muhimu na haraka.. msimamo wa Marjaa Dini mkuu kuhusu maandamano yanayo endelea ya kudai islahi.

Maoni katika picha
Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa ya leo (17 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (15 Novemba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) amesoma nakala kutoka ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu.

Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesema: Enyi mabwana na mabibi.. tunakusomeeni nakala iliyotufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani katika mji mtukifu wa Najafu.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Kwa mara nyingine Marjaa Dini mkuu anaeleza msimamo wake kuhusu maandamano yanayo endelea ya kudai islahi kupitia nukta kadhaa:

Kwanza: kuunga mkono maandamano na kusisitiza yafanyike kwa amani, yasiwe na uvunjifu wowote wa amani, tunalaani kuwafanyia uwadui watu wanaofanya maandamano ya amani kwa kuwaua, kuwajeruhi, kuwateka, kuwafukuza na mengineyo, pia tunalaani kuwafanyia uwadui askari na kuharibu mali za serikali na za watu binafsi, anapaswa kuchukuliwa hatua kila atakaye fanya hayo, -ni haram kisheria na kinyume cha katiba- watu hao wanatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sharia, wala haifai kuwaacha wahalifu hao.

Pili: hakika uhalali wa serikali unategemea wananchi, hakuna anayeipa haki kisheria zaidi ya mwananchi, matakwa ya raia huonekana kupitia matokeo ya uchaguzi huru na wa haki, hakika ni muhimu kutengeneza haraka kanuni za uchaguzi huru na wa haki utakao rudisha uwaminifu kwa wananchi bila kuwepo kwa upendeleo wa vikundi fulani au vyama vya kisiasa, itolewe nafasi ya mabadiliko ya kweli yatakayo onyesha tofauti kati ya serikali hiyo mpya na zilizo pita, kama raia watapenda kubadilisha viongozi wapya, kupitia uchaguzi huru na wa haki utakao kubaliwa na raia.

Tatu: pamoja na kupita muda mrefu tangu kuanza maandamano ya wananchi wanao dai islahi, na damu tukufu iliyo mwagika ya mamia ya mashahidi na maelfu ya majeruhi, bado hadi leo matakwa ya waandamanaji hayaja fanyiwa kazi, hasa upande wa kuwawajibisha mafisadi wakubwa na kurudisha mali za taifa, na kuondoa upendeleo kwa baadhi ya vikundi, jambo linalo tia shaka kuhusu dhamira ya viongozi wa kisiasa katika kutekeleza madai ya waandamanaji na kufanya mabadiliko ya kweli chini ya uongozi wao.

Nne: wananchi hawajatoka kwenda kwenye maandamano kudai islahi (mabadiliko) kwa namna hii hapo awali, wala hawajawahi kuandamana kwa muda mrefu kiasi hiki, pamoja na kupata mitihni mingi kwenye maandamano haya lakini bado wamesimama imara na wanaendelea kuongezeka siku baada ya siku, kutokana na watawala wa serikali kulifanya taifa kama mali yao, wanagawana utajiri wa taifa na kufumbia macho ufisadi, hadi wamelifikisha mahala pasipo vumilika, na imekua vigumu kwa mwananchi wa kwaida kupata mambo madogo ya msingi katika maisha, pamoja na utajiri mkubwa wa taifa hili. Kama watawala bado wanafikiri kuwa wanaweza kukwepa kufanya mabadliko ya kweli wajuwe wanajidanganya, baada ya maandamano haya haiwezekani hali ikawa kama ilivyo kua awali, wanatakiwa watambue hilo.

Tano: hakika vita ya islahi inayo ongozwa na raia wa Iraq, ni vita ya kitaifa inayo wahusu wananchi peke yake, wairaq ndio wanaopaswa kubeba machungu ya vita hii, haifai kuruhusu kuingiliwa na mtu yeyote wa nje, kuingiliwa na watu wa nje ni hatari kubwa, kutalifanya taifa kuwa uwanja wa vita na sehemu ya kutekeleza matakwa ya nchi za kigeni na muathirika mkubwa atakua ni raia wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: