Misikiti ni nyumba za Mwenyezi Mungu mtukufu, ametaja utukufu wake katika aya ishirini na nane ndani ya kitabu chake kitakatifu, tena kaegemezea kwake kuonyesha heshima na utukufu wake, anasema: (Hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu msimuombe yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu), amesisitiza ujenzi wa misikiti, na akasema wanaojenga misikiti ndio wanao muamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, misikiti ni nyumba za ibada, dhikri na kumnyenyekea Mwenyezi Mungu mtukufu, kutokana na utukufu huo miongoni mwa machapisho ya kitengo cha Dini yaliyopata mwitikio mkubwa ni kitabu cha (Adabu na hukumu za misikiti), kimebainisha adabu na hukumu za misikiti kwa mujibu wa aya za kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu na hadithi za Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Kitabu hiki kinamilango kadhaa, ambayo ni:
- - Ubora wa swala ya jamaa.
- - Ubora wa kuingia msikitini.
- - Karaha za kuchelewa kuingia msikitini kwa mtu anayeishi jirani na msikiti.
- - Yanayo suniwa wakati wa kuingia msikitini.
- - Yanayo chukiza (makuruhu) wakati wa kuingia msikitini.
Kutokana na kukubalika kwa kitabu hiki kimesha chapishwa mara kadhaa, hadi sasa kinapatikana katika duka la kitengo cha Dini mkabala na mlango wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na unaweza kukipakua katika ukurasa wa kitengo cha Dini kwenye mtandao maalum kupitia link ifuatayo:
https://alkafeel.net/religious/index.php?iss
Kumbuka kua kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesha chapisha vitabu kadhaa vyenye ukubwa mbalimbali na masomo tofauti, kama vile Fiqhi, Aqida, Akhlaq, Jamii, waandishi wake wanatumia lugha rahisi ianayo eleweka na kila mtu, na kuweka ushahidi wa aya za Quráni na hadithi za Mtume pamoja na Maimamu wa Ahlulbait (a.s).