Chuo cha Al-Ameed kinaunga mkono maandamano ya amani

Maoni katika picha
Hali yake sawa na taasisi zingine za kisekula hapa Iraq na kigezo cha wafanyakazi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu kimetangaza kuunga mkono watu wanaofanya maandamano ya amani na kudai haki zao walizo pewa kikatiba na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu.

Wanafunzi wa chuo hicho wameingia barabarani kuunga mkono maandamano ya amani yaliyo anza mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba.

Katika matembezi hayo wamewaombea dua watu walio uwawa kwenye maandamano, na wamesoma risala kutoka kwa Mheshimiwa rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali, pamoja na makamo kiongozi dokta Alaa Mussawi na wakuu wa vitengo (vitivo) sambamba na viongozi wa vitengo na idara za chuo.

Chuo na wanafunzi wake hawajaishia kufanya vivyo peke yake, wameshiriki pia katika uwanja wa maandamano na kutoa huduma za matibabu na zinginezo kwa watu wanaofanya maandamano ya amani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: