Kama sehemu ya wajibu wao katika kuhuisha matukio ya furaha, sikukuu na tarehe za kuzaliwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), Masayyid wanaofanya kati katika Atabatu Abbasiyya wamewapokea watu wanaokuja kutembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kutumia maneno mazuri na kuwapongeza kwa kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s), pamoja na kugawa halwa kwa kila zaairu.
Kiongozi wa idara ya wafanyakazi ambao ni masayyid, Sayyid Hashim Shami ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaharakati nyingi, miongoni mwa harakati zao ni kuadhimisha tarehe walizo zaliwa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), ikiwa ni pamoja na siku aliyozaliwa muokozi wa walimwengu Mtume Muhammad (s.a.w.w) inayo fungamana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mjukuu wake Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s), kwa lengo la kuadhimisha siku hiyo aidha kutokana na utukufu wake watumishi wa idara hii wamewekwa kwenye milango ya Ataba tukufu, kwa ajili ya kuwapokea mazuwaru kwa maneno mazuri na kuwapa halwa”.
Akaongeza kua: “Tumegawa zaidi ya vipande (8000) vya halwa, kitendo hicho kimefurahiwa sana na mazuwaru, wamewashukuru wasimamizi wa ratiba hiyo, wamesema kua pamoja na udogo wake lakini imewaachia athari kubwa katika nyoyo zao”.