Shule za Al-Ameed ambazo zipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zimeratibu matembezi ya kuunga moko watu wanaofanya maandamano ya amani na kudai haki zao, kutokana na mapenzi yao kwa taifa na uzalendo wao.
Matembezi hayo wameshiriki wanafunzi na watumishi wa shule za Al-Ameed, yamepambwa na mimbo ya kizalendo pamoja na madai ya islahi, sambamba na maigizo yanayo onyesha uzalendo wa taifa lao na madai ya waandamanaji ya kutaka maisha bora na mustakbali mwema kwa wairaq wote.
Kumbuka hua matembezi haya yanatokana na kutekeleza maagizo ya Marjaa Dini mkuu, ambaye anapaza sauti mara nyingi ya kutaka mabadiliko (islahi), kupitia khutuba za Ijumaa na maelekezo mbalimbali anayo toa kupitia Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji mtukufu wa Karbala.