Hospitali ya rufaa Alkafeel imetoa matibabu bure kwa zaidi ya waandamanaji (800) wakiwemo (86) waliokua katika hali mbaya, kuna ambao wamepokelewa moja kwa moja katika hospitali hiyo wengine wamepelekwa na gari za wagonjwa huku wengine wakitokea kwenye vituo vya afya vilivyo funguliwa katika uwanja wa maandamano katikati ya mji wa Karbala.
Jambo hili ni miongoni mwa juhudi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuwasaidia watu wanaofanya maandmano ya amani kudai haki zao kisheria walizo pewa na katiba na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu, pia ni sehemu ya ujumbe wa kibinaadamu unao onyeshwa na wafanya kazi wa hospitali.
Uongozi wa hospitali umesema kua umefungua vituo vya afya katikati ya mji wa Karbala, na wameshatoa huduma za afya kwa zaidi ya waandamanaji (800) tangu kuanza maandamano, na bado wanaendelea kutoa huduma hadi sasa.
Asilimia kubwa ya watu waliopewa huduma za matibabu ni wale walio athiriwa na gesi ya kutoa machozi na waliokua na majeraha madogo na saizi ya kati, pia wapo waliokua wameshambuliwa kwa risasi, jumla ya watu (86) walikua na hali mbaya, miongoni mwao (6) ni askari, wote walibebwa na magari ya wagonjwa hadi hospitalini kwa matibabu zaidi.
Majeruhi wote waliruhusiwa baada ya kupewa matibabu na kupata nafuu, ispokua wawili tu ndio bado wamelazwa hospitali chini ya uangalizi maalum na mwingine kafanyiwa upasuwaji.