Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetoa maelekezo mapya ya kuwarudisha wapiganaji wake kazini.

Maoni katika picha
Uongozi wa kikosi cha Abbasi (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) umetoa maelekezo mapya ya kurudisha wapiganaji wake kazini.

Umesema kua: Wapiganaji wote wenye sifa zitakazo tajwa hapo chini, wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja viambatanisho vyao na picha mbili ndogo, katika kamati maalum kwenye makao makuu ya kikosi cha Abbasi (a.s), yaliyopo Karbala/ barabara ya Istiratiji/ karibu na kiwanda cha Sharmastuun, hadi tarehe 25/11/2019m, ofisi zipo wazi saa mbili asubuhi hadi saa tisa Alasiri.

Masharti:

  • 1- Awe mtu aliyejitolea kupigana katika kikosi hiki, awasilishe ushahidi wowote unao thibitisha ushiriki wake katika matukio manne kwa uchache.
  • 2- Awe mpiganaji wa zamani wa kikosi hiki au Hashdi Difai na aliwahi kupokea japo mshahara mmoja katika kikosi hiki kwa uchache.
  • 3- Jina lake liwepo katika orodha ya wapiganaji wa kikosi, hata lisipo onekana katika cd za Hashdi Sha’abi, ukitoa wale walio simamishwa kazi katika vikao vya uhakiki au kutokana na makosa ya kiaskari.

Fahamu kua kikosi kinakamilisha utaratibu wa kuwarudisha wapiganaji wake kazini na kuwapeleka kwenye sekta husika, kwa ajili ya kukamilisha taratibu za malipo na kutekeleza majukumu ya kiofisi watakayo elekezwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: