Sauti ya raia: Haya ndio yaliyosemwa na Marjaa Dini mkuu tarehe (23/ 9/ 2011m).

Maoni katika picha
Kwa miaka mingi wanasiasa waliziba masikio yao, hawakutaka kusikia maelekezo na nasaha za Marjaa Dini mkuu, amekua akitoa nasaha na maelekezo kwa kila aliyepata nafasi ya uongozi serikalini kwa kipindi kirefu, aliwasisitiza waache marumbano baina yao na kuweka mbele maslahi ya taifa, na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.

Katika khutuba ya Ijumaa ya mwezi (24 Shawwal 1432h) sawa na (23/ 9/ 2011m) iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s), Marjaa Dini mkuu alisisitiza kua jambo haliishii kwenye kutoa nasaha na maelekezo peke yake, kama hakuna anayesikiliza na kufanyia kazi hakuna faida ya nasaha hizo.

Ifuatayo ni sehemu ya yaliyo elezwa katika khutuba hiyo, Shekh Karbalai alisema kua: “Swala la wanasiasa kuhitaji nasaha za Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani, kuwa baadhi ya wanasiasa wanahitaji nasaha zake kwa sasa. Nawajibu kua nasaha peke yake hazitoshi kumaliza matatizo ya nchi, Mheshimiwa amesha toa nasaha na maelekezo mara nyingi siku za nyuma, kama wanasiasa wangefanyia kazi maelekezo hayo tungekua katika hali nzuri hivi sasa, nasaha na maelekezo bila kufanyiwa kazi hakuna faida, tunahitaji viongozi wa serikali wanao tanguliza maslahi ya taifa lao, sio maslahi binafsi au ya chama au kikundi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: