Idara imesema kua tangu yalipo anza maandamano imekua mstari wa mbele kusaidia waandamanaji, ilianza kufanya hivyo katika uwanja wa uhuru huko Bagdad, kisha wakaenea kwenye mikoa mingine, miongoni mwa huduma wanazo toa ni:
- - Kujenga vituo vya kutoa huduma.
- - Kuandaa chakula na kukigawa kwa waandamanaji.
- - Kugawa chakula, maji na juisi kwa waandamanaji.
- - Kutoa huduma za matibabu kwa majeruhi.
- - Kuandaa gari za wagonjwa na kutoa huduma ya kwanza ya matibabu.
- - Msaada wa kimkakati na kuhakikisha mawakibu nyingi zinakuwepo katika uwanja wa maandamano.
- - Kugawa baadhi ya vifaa vinavyo tumiwa na waandamanaji.
- - Kushiriki katika makundi ya kujitolea kufanya usafi na kazi zingine.