Tangazo la mashindano ya kuhifadhi Duau-Tawassul.

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza mashindano ya kuhifadhi Duau-Tawassul iliyo pokewa kutoka kwa Maimamu (a.s), ambayo inaanza kwa (Allahumma innii as-aluka wa atawajjahu ilaika binabiyyika Nabiyyi Rahmah…) iliyopo katika kitabu cha Mafatihi Janani, mashindano yanahusu wanawake tu, wa umri wowote.

Kila anayependa kushiriki aende kwenye kituo cha Swidiiqah Twahirah katika mkoa wa Karbala/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya Hospitali ya Husseini, siku ya Jumanne sawa na (10/12/2019m) saa tatu asubuhi kwa ajili ya kufanya mtihani, kutakua na zawadi kwa washindi watakao patikana baada ya kupiga kura.

Masharti ya shindano ni:

  • 1- Kuhifadhi dua yote kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Mafatihu Jinani.
  • 2- Kuandika kwa hati nzuri inayo someka pamoja na kuweka shikli.
  • 3- Muta wa mtihani ni saa moja tu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na kituo kupitia namba za simu zifuatazo:

  • - (07828884555) kwa Viber, Whatsapp na Telegram.
  • - (07730124335) / (07730134335) kwa Whatsapp.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: