Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika siku ya elimu ya kumi na nne katika hospitali ya Hindiyya.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika sherehe za siku ya elimu ya kumi na nne kwenye hospitali ya Hindiyya (kitengo cha kutibu maradhi sugu ya watoto), iliyo fanywa na hospitali hiyo asubuhi ya Jumatano (22 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (20 Novemba 2019m), ndani ya hoteli ya Barun Karbala, chini ya kauli mbiu isemayo: (Kwa elimu na kazi tunajenga Iraq bora na imara).

Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya ilikua unahusu namna ya kubaini tatizo la upweke na jinsi ya kulitibu bila kutumia dawa, mada hiyo iliwasilishwa na muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya nchini Marekani Dokta Shaamil Muhsin Haadi, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kongamano hili linasimamiwa na hospitali ya Hindiyya katika mji mtukufu wa Karbala, na kualikwa Atabatu Abbasiyya ili kueleza tatizo la maradhi ya upweke”.

Akaongeza: “Daima Atabatu Abbasiyya hushiriki katika makongamano na mikutano ya aina hii, kwa ajili ya kuhamisha uzowefu wa baadhi ya mambo yanayo fanywa na nchi zilizo endelea”.

Akafafanua kua: Ushiriki wetu wa leo umejikita katika kuelezea tatizo la maradhi ya upweke, tumefafanua namna ya kubaini maradhi hayo na kuyatibu bila kutumia dawa, kwani watoto wengi wanapata tatizo hilo”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya warsha na nadwa nyingi zinazo husu afya kupitia taasisi zake za tiba katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: