Atabatu Abbasiyya kwa mara ya kwanza hapa Iraq tena kwa hati ya kiiraq imetoa msahafu wa tajwidi.

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa mafanikio ya miradi adim ya Quráni, kituo cha maarifa ya Quráni na kuifasiri chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoka msahafu wa tajwidi wa rangi ulio andikwa kwa hati ya kiiraq chini ya usimamizi wa kamati maalum.

Mkuu wa kituo hicho Shekh Dhiyaau-Dini Zubaidi ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu toleo hilo, amesema kua: “Hakika msahafu unao ngára hivi sasa ni matokeo ya msaada wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kituo cha Quráni tukufu, hii ni sehemu ya mafanikio yaliyo patikana”.

Akasema kua sifa za msahafu huu ni:

  • - Umechapishwa katika kiwanda cha Darul-Kafeel kwa karatasi bora na uchapaji wa fahari.
  • - Umeandikwa na muiraq Hamidi Saadi kwa kushirikiana na muiraq mwingine Sayyid Muhammad Mushrafawi.
  • - Rangi zake zimeongeza uzuri sambamba na uzuri wa mpangilio na usanifu.
  • - Umewekwa nakshi zilizo ongeza uzuri na muonekano.
  • - Umeandikwa kwa hati ya (Naskhi) ambayo inamuonekano mzuri na inasomeka kwa urahisi.
  • - Umewekwa alama na ishara zenye rangi maalum katika elimu ya tajwidi.
  • - Haraka zake ziko wazi kwa mwenye kutaka kujifunza usomaji na tajwidi kwa ufasaha.
  • - Umehakikiwa na kupasishwa na jopo la watalamu wenye weledi mkubwa wa mada, lugha, tafkhim na mengineyo.
  • - Msahafu wa tajwidi ni muongozo kwa kila anayetaka kujifunza usomaji sahihi wa Quráni tukufu.
  • - Msahafu wa tajwidi umebainisha hukumu za usomaji na tajwidi kwa njia rahisi kupitia alama zilizopo chini ya kurasa, kila rangi inawakilisha hukumu ya tajwidi ndani ya Quráni tukufu.

Kumbuka kua kituo cha maarifa ya Quráni kuifasiri na kuichapisha ni moja ya vituo muhimu katika Maahadi ya Quráni tukufu, na kimesha fanya miradi mingi ya Quráni, inayo saidia kueneza utamaduni wa Quráni, ikiongozwa na mradi wa kuchapisha msahafu maalum wa Atabatu Abbasiyya tukufu, nayo ni mafanikio makubwa katika fani ya Quráni, kwa sababu ndio msahafu wa kwanza kuchapishwa hapa Iraq, kazi hiyo ilikua inafanywa na taasisi za Quráni nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: