Kupenda taifa ni katika imani: Shule za Al-Ameed zimejikita katika kufundisha uzalendo kwa wanafunzi wake kupitia kuwaunga mkono watu wanaofanya maandamano ya amani

Maoni katika picha
Kupenda taifa na kujitolea kwa ajili yake ndio msingi unaofanyiwa kazi na shule za Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuufundisha uzalendo huo kwa wanafunzi wake, jambo hilo limeonekana katika harakati kadhaa zinazo fanywa na idara za shule za Al-Ameed, kwa kuwaunga mkono watu wanaofanya maandamano ya amani kudai mabadiliko (islahi) na maisha bora na huru.

Miongoni mwa mambo yanayo fanywa na shule za Al-Ameed ni kuwaunga mkono watu wanaofanya maandamano ya amani, wanafanya hivyo kwa kuimba mimbo inayo onyesha uzalendo wa taifa na raia wake watukufu, sambamba na kufanya maigizo ya uzalendo.

Hawajaishia kuonyesha mambo ya kishule peke yake, bali wamefanya matembezi hadi kwenye uwanja wa maandamano katikati ya mji mtukufu wa Karbala, huku wakiwa wamebeba bendera za Iraq na kupiga yowe za kutaka mabadiliko na heshima ya taifa.

Miongoni mwa shughuli zinazo fanywa na wanafunzi wa shule za Al-Ameed ni kwenda katika mabanda ya Atabatu Abbasiyya yaliyopo karibu na uwanja wa maandamano na kuwasaidia watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kugawa chakula na vinywaji kwa waandamanaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: