Katika khutuba ya Ijumaa (22 Dhulqadah 1432h) sawa na (21/10/2011m) iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmhadi Karbalai ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), alieleza mambo kadhaa muhimu na matarajio ya wananchi wa Iraq, miongoni mwa mambo hayo ni:
- 1- Matumizi ya pesa yaelekezwe kwenye kujenga nyumba za makazi, jambo hilo litasaidia kuboresha huduma kwa raia.
- 2- Kuwatumia watalamu wasiokua na ajira katika miradi inayo hitajiwa na raia.
- 3- Kuboresha sekta ya viwanda, kilimo, utumishi, utalii na zinginezo.
- 4- Kuwa na utashi thabiti na maamuzi imara ya kupambana na ufisadi katika vyama vya kisiasa.
- 5- Tunahitaji kurekebisha taratibu za kiutawala kwa kufanyia marekebisho sheria za zamani na kuondoa vipengele vinavyo kwamisha maendeleo na kuzuwia wawekezaji kuja Iraq.
- 6- Lazima kuwe na utaratibu wa wazi na adilifu katika uteuzi wa nyadhifa serikalini, wala sio kwa ujamaa na undugu.
- 7- Kipaombele iwe kupunguza ufakiri Iraq hasa kwa wajane na mayatima, watu ambao wanaongezeka kila siku kutokana na matatizo yanayo endelea hapa nchini.