Viongozi wa hema hilo wamesema kua wamefungua hema hili kwa ajili ya kuwafundisha waandamanaji jinsi ya kusaidia majeruhi wa aina mbalimbali, pia mafunzo haya yanasaidia kutambua namna ya kujikinga na hatari, wanawafanya waweze kuokoa nafsi zao na watu wengine pia.
Mafunzo yamejikita katika kufundisha namna ya kutoa msaada wa haraka kwa muathirika na kumpa mahitaji ya lazima hadi atakapo fikishwa sehemu anayo weza kupewa matibabu kamili.
Mafunzo yapo ya nadhariya na vitendo, yanahusu namna ya umuokoa mtu aliyeshambuliwa au aliyepata mshtuko wa moyo, aliye athirika na mabomu ya machozi na mengineyo.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa misaada mbalimbali kwa waandamanaji, miongoni mwa misaada hiyo ni:
- - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula kupitia mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kuwatumia kwa gari maalum.
- - Kugawa maelfu ya chupa za maji safi ya kunywa.
- - Kugawa juisi, matunda na chai kwa nyakati tofauti.
- - Kufanya usafi katika maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji kwa kutumia gari maalum za usafi.
- - Kufungua vituo maalum vya kugawa maji kwa waandamanaji.
- - Kutoa matibabu bure kwa waandamanaji na askari wanaopata matatizo ya afya katika hospitali ya rufaa Alkafeel.