Wito kwa wanawake wa kushiriki na kunufaika na program ya (Mafatihu Saádah).

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ambacho kinalenga kujenga utulivu wa nafsi katika familia za Iraq, katika kuendelea kutekeleza shughuli zake zinazo kusudia kufikia lengo la kuanzishwa kwake, kinatangaza kuendesha program ya (Mafatihu Saádah) kwa ajili ya kuwafunda (kuwafundisha) wasichana wanaokaribia kuolewa miongoni mwa wanafunzi wa vyuo, wafanya kazi na wahitimu wa masomo mbalimbali, kinatoa wito kwa kila anayetaka kushiriki mafunzo haya adhimu ya kujenga familia bora yenye mshikamano.

Kituo kimesema kua program inahatua tatu:

Hatua ya kwanza: mafunzo ya siku tatu (3) katika kila mwezi.

Hatua ya pili: mafunzo ya siku tano (5) katika kipindi cha likizo.

Hatua ya tatu: inawahusu wasichana (waliochumbiwa na wenye ndoa mpya) kwa muda wa siku nne (4) katika kipindi cha likizo za kiangazi.

Kila anayependa kushiriki atume (jina lake, umri na kiwango cha elimu yake) kupitia namba zifuatazo: (07828884555 / 07730134335 / 07730124335) kwa Viber, Whatsapp au Telegram.

Kituo kipo mtaa wa Mulhaq/ barabara ya hospitali ya Hussein (a.s), kimeandaa usafiri wa washiriki kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala, pamoja na malazi na chakula kwa wale watakao toka nje ya mkoa wa Karbala, sambamba na masomo hayo, kutakua na ratiba za ziada kama vile kufanya ziara katika ataba takatifu na kutembelea maeneo ya Atabatu Abbasiyya tukufu na miradi yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: