Baada ya kumaliza ukarabati: jengo la vyoo katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) limeingizwa katika utowaji wa huduma.

Maoni katika picha
Jengo la vyoo katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limeanza kufanya kazi, baada ya kumaliza ujenzi kwenye jengo hilo, na kuliweka katika muonekano mpya unao endana na uboreshwaji wa Maqaam hiyo.

Jengo hilo limechukua nafasi ya jengo la vyoo la zamani lililokua na mapungufu mengi, pia limedumu miaka mingi pamoja na udogo wake na kutokua na matundu ya vyoo ya kutosha, ndipo ikaamuliwa ufanyike ujenzi wa jengo hili jipya kwa ajili ya kuboresha huduma kwa watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), aidha ni muendelezo wa miradi ya ujenzi inayo endelea katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f).

Jengo linaukubwa wa mita za mraba (222) lina sehemu mbili, sehemu ya wanaume na wanawake, kila sehemu ina vyoo (16) na imefungwa mitambo ya kusafisha hewa, pia muonekano wake wa nje umepambwa kwa marumayu sambamba na kuwekwa viyoyozi.

Fahamu kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kina nafasi kubwa katika ujenzi wa vyoo ndani na nje ya Ataba kutokana na mafundi mahiri kilionao, waliobobea katika fani zote za ujenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: