Kazi inaendelea ya kuweka mapambo na nakshi kwenye mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Mafundi na wahandisi wanaendelea na kazi ya kuweka mapambo na nakshi kwenye mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wanakamilisha kazi waliyo anza siku nyingi na imepiga hatua kubwa, chini ya utaratibu na muda uliopangwa.

Kazi iliyokamilika ni nzuri sana, mbele ya mlango wa kuingia katika haram ya Abbasi imepambwa na kuwekwa nakshi nzuri zinazo endana na utukufu wa eneo hilo.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, amesema kua: “Tumemaliza sehemu nyingi za kazi hii, baadhi ya sehemu zimekamilika kabisa na sehemu zingine kazi inaendelea, tumemaliza kuweka mapambo na nakshi katika mlango wa Kibla, kuna mapambo ya nusu duara sita yaliyo nakshiwa vizuri na kuwekwa Kashi Karbalai, zinafuatiwa na nusu duara zingine tatu zenye ufito wa dhahabu halisi, kila nusu duara imeandikwa aya za Quráni, na upande wa ndani kuna ufito wa maandishi ya aya za Quráni pia, mapambo hayo yapo kwa nje na ndani, aidha kuna maandishi ya Quráni kwa juu yake”.

Akendelea kusema kua: “Tumemaliza kuweka Kashi Karbalai kwa ndani iliyo tiwa dhahabu, hii ni mara ya kwanza kutumiwa Kashi za aina hiyo, kutokana na umaalum wa mlango huo, pia tumekamilisha sehemu kubwa ya mapambo na nakshi, kazi hii inafanywa sambamba na kazi zingine ambazo zimepiga hatua kubwa.

Kumbuka kua mradi huu ni sehemu ya mradi mkubwa wa upanuzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambapo milango ya Ataba imeongezwa ukubwa mara kadhaa tofauti na ilivyokua mwanzo, na kuwekwa nakshi na mapambo mazuri kulingana na nafasi ya kila mlango, ili kuwezesha kuingia kwa urahisi idadi kubwa ya mazuwaru na mawakibu husseiniyya, kazi ya upanuzi wa milango hiyo imesanifiwa na kutekelezwa na shirika la ujenzi la Ardhi takatifu chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, utengenezaji wa milango hiyo unahitaji umakini na ustadi wa hali ya juu, kwa hiyo kazi hiyo ilihitaji muda mrefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: