Mradi wa (Nyumba za makazi Alwafaa) kwa ajili ya familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) umepiga hatua kubwa.

Maoni katika picha
Kutokana na msaada wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi ya ujenzi wa nyumba za makazi Alwafaa (Daru Ummul-Banina –a.s-), nyumba maalum za kuishi familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s), kama sehemu ya kuonyesha thamani ya kujitolea kwao kwa ajili ya taifa la Iraq na maeneo matakatifu.

Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/ 26 Hashdi Shaábi) kimesema kua kazi ya ujenzi inaendelea,: “Mradi huo unajengwa katika mji wa Karbala – mtaa wa Mulhaq Alfaaris- umesha piga hatua kubwa, kwa ajili ya kuzienzi familia za mashahidi watukufu”.

Akaongeza kua: “Hakika uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) unataka kutoa nyumba kwa kila familia ya shahidi wa Alkafeel, pamoja na wapiganaji wake wengine, zitajengwa nyumba zingine katika mikoa mingine pia”.

Ustadh Maitham Zaidi kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji amesema kua: “Tunapenda kutoa nyumba kwa kila familia ya shahidi wa Hashdi Shaábi na wapiganaji walio itikia wito wa Marjaa Dini mkuu, hii ni hatua ya kwanza ya ujenzi wa nyumba za kuishi familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika mtaa wa Mulhaq hapa Karbala”.

Tambua kua mradi huu ni sehemu ndogo sana ya kuonyesha shukrani kutokana na namna walivyo jitolea mashahidi pamoja na familia zao kwa ajili ya kulinda taifa la Iraq na raia wake pamoja na maeneo matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: