Katika uwanja wa uhuru wa Karbala hadi uwanja wa uhuru wa Bagdad: Atabatu Abbasiyya tukufu yaonyesha uwepo wake na kusaidia waandamanaji.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu bado inaendelea kusaidia waandamanaji wanaodai haki walizo pewa na katika na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu, imekua ikitoa misaada ya aina mbalimbali, baada ya kusaidia waandamanaji katika uwanja wa uhuru wa Karbala, ambapo imekua ikitoa chakula, matibabu na mengineyo, sasa wameanza kutoa misaada katika uwanja mkubwa zaidi wa waandamanaji ujulikanao kama (uwanja wa uhuru) katikati ya mji mkuu wa Bagdad, imeonyesha uwepo wake na kutoa inacho weza kusaidia.

Miongoni mwa vitu inavyo toa ni maji na chakula vikavu vya aina tofauti, waandamanaji wamepongeza na kusifu uwepo wake, kazi ya kugawa maji na chakula hicho imesimamiwa na wafanyakazi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), tunategemea kuendelea kusaidia siku zijazo.

Kumbuka kua miongoni mwa vitu vilivyo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu ni:

  • - Kuandaa chakula katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya na kwenda kukigawa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji ya kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa wakati tofauti kwa waandamanaji.
  • - Kufanya usafi katika maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji kwa kutumia gari maalum za usafu.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji kwa waandamanaji.
  • - Kutoa huduma za matibabu bure kwa kila mtu anayepata tatizo la kiafwa kwenye mandamano sawa awe raia au askari.
  • - Hema la kutoa mafunzo ya huduma ya kwanza, sambamba na kuwafundisha waandamanaji mbinu za uwokozi, pamoja na kutoa huduma ya uokozi kwa waandamanaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: