Sauti ya raia: Haya ndiyo yaliyosemwa na Marjaa Dini mkuu tarehe (16/12/2011m).

Maoni katika picha
Mara nyingi na kabla ya kupangwa bajeti yeyote ya taifa, Marjaa Dini mkuu alikua anahusia kupewa kipaombele huduma za kijamii na kupambana na ukosefu wa ajira, akatoa maelekezo mazuri na akashauri kuacha kutegemea mafuta kama pato pekee la taifa, kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa taifa.

Tunataja aliyosema Marjaa Dini katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) (20 Muharam 1433h) sawa na (16/12/2019m) iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai.

Kuhusu bajeti ya mwaka (2012m) iliyokua inawasilishwa bungeni wakati huo, alihusia umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo kati ya kamati ya mali bungeni pamoja na baraza la mawaziri, kuhusu umuhimu wa kuendeleza sekta ya viwanda, kilimo na utalii wa kidini, wala wasiendelee kutegemea mafuta kama pato pekee la taifa, kwa sababu zifuatazo:

  • 1- Pato la mafuta linategemea huruma ya soko la mafuta la dunia, bie yake hubadilika mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya uchumi wa dunia jambo linalosababisha kutokua na uchumi tulivu hivyo kuathiri maendeleo ya taifa.
  • 2- Kushughulikia tatizo la ukosefu wa ajira kwa kuboresha sekta ya viwanda, kilimo na utalii.
  • 3- Kutumia wasomi na wabunifu wazalendo.
  • 4- Kujenga uchumi wa kujitegemea na kuepuka uchumi tegemezi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: