Gari za wagonjwa ambazo zipo chini ya hospitali ya rufaa Alkafeel zina kuzi kubwa na muhimu, zinabeba watu wanaojeruhiwa kwenye maandamano katika mji wa Karbala, wamesha beba makumi ya majeruhi na kuwapeleka hospitalini kwa ajili ya kupewa matibabu.
Muda wote gari za wagonjwa za hospitali ya Alkafeel zimesimama karibu na vituo vya afya katika uwanja wa waandamanaji mjini Karbala hadi usiku wa manane, kwa ajili ya kutoa msaada kwa mtu yeyote atakaye pata tatizo la kiafya na kumpeleka hospitali haraka.
Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ilitoa na bado inaendelea kutoa huduma za afya bure kwa watu wanaojeruhiwa kwenye maandamano mjini Karbala, inapokea wagonjwa kila siku, imeandaa timu maalum ya madaktari na wauguzi kwa ajili ya kuhudumia watu wanaojeruhiwa kwenye maandamano kwa haraka.