Katika kuunga mkono maandamano: Atabatu Abbasiyya tukufu yafunga vipaza sauti kwenye uwanja wa Tarbiyya.

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya kwenye uwanja wa maandamano ya amani mjini Karbala, idara ya vipaza sauti chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefunga vipaza sauti kwenye uwanja wa Tarbiyya walipo weka kambi waandamanaji.

Vipaza sauti vimewekwa kwa mpangilio mzuri unaowezesha sauti kusikika maeneo yote ya uwanja huo, lengo la hatua hiyo ni kuweza kutoa maelekezo kwa waandamanaji, sambamba na kuhakikisha maandamano yanafanyika kwa amani na kwa mpangilio.

Tambua kua tangu yalipo anza maandamano hapa Iraq na katika mji wa Karbala, Atabatu Abbasiyya tukufu haija acha kuwahudumia waandamanaji, sio kwamba inahudumia waandamanaji wa Karbala peke yake, bali nametuma misafara ya kutoa huduma hadi katika mji mkuu wa Bagdad makao makuu ya maandamano kwenye uwanja wa uhuru, wamegawa kiasi kikubwa cha maji na chakula.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: