Marjaa Dini mkuu amehimiza mara nyingi umuhimu wa kuheshimu sheria na kufanyiwa kazi, sio kama inavyo tokea mara nyingi, sheria zinatungwa lakini hazifanyiwi kazi, akasema kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Tunajikumbusha baadhi ya aliyosema kwenye khutuba ya Ijumaa ya mwezi (5 Safar 1433h) sawa na (30 Desemba 2019m), iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s), alisema kua: “Kuna jambo muhimu yafaa lizingatiwe, nalo ni kwamba sheria yenyote itakayo tungwa na kupasishwa na bunge kisha kutangazwa kwenye magazeti lazima itekelezwe, sio kama ilivyo tokea katika sheria ya kupunguza mishahara ya wakuu watatu wa nchi, pamoja na kupasishwa na bunge sharia hiyo na kutangazwa kwenye magazeti lakini bado haijatekelezwa!! Pamoja na kwamba imepitishwa kutokana na msukumo mkubwa wa wananchi pamoja na Marjaiyya, lakini ilipo fika kwenye meza ya utekelezaji, haijatekelezwa!! Bali wanataka kuifanyia marekebisho”.
Akauliza kua: “Jambo hili sio uvunjaji wa sheria?!”, akaongeza kua: Kwa nini serikali inataasisi ambazo haziheshimu sheria?! Tena sheria zilizo tungwa kwa msukumo wa wananchi, kwa nini zisiheshimiwe?.