Shindano la kisa kifupi cha Zainabiyya kwa wanawake na wito wa kishiriki kwenye shindano hilo.

Maoni katika picha
Shindano linalenga kuangazia nafasi ya bibi Zainabu (a.s) katika kunusuru mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s), kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya kimetangaza shindano la kuandika kisa kifupi kwa jina la (shindano la kisa cha Zainabiyya), chini ya mada zifuatazo:

  • 1- Nafasi ya bibi Zainabu (a.s) katika habari.
  • 2- Subira ya bibi Zainabu (a.s).
  • 3- Msimamo wa bibi Zainabu (a.s).
  • 4- Ufasaha wa bibi Zainabu (a.s).
  • 5- Makuzi ya bibi Zainabu (a.s) na uhusiano wake kifamilia na kijamii.

Kituo kimetoa wito kwa kila anayependa kushiriki atume kisa chake kwenye ukurasa wa kituo katika (facebook) sehemu ya barua, chini ya masharti yafuatayo:

  • - Kisa kiandikwe kwa kutumia program ya (word) na itumwe kwenye namba (07828884555/ telegram), au kwenye barua pepe ifuatayo: thaqafaasria@gmail.com.
  • - Maneno yasiwe chini ya (500) na yasizidi (1000).
  • - Kisa kisiwe kipo kwenye mtandao wowote wala kisiwe kimesha wahi kuandikwa sehemu yeyote.
  • - Uandishi uchunge kanuni za lugha nahau na imla.

Kituo kimesema kua matokeo yatatangazwa na kutoa zawadi kwa washindi katika tarehe ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s), mwezi tano Jamadal-Ula (1441h) sawa na (1/1/2020).

Kumbuka kua kituo cha utamaduni wa familia kinaangalia utamaduni wa familia na jamii, kipo katika mkoa mtukufu wa Karbala/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya hospitali ya Hussein (a.s) ndani ya jengo la kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s). kwa maelezo zaidi piga simu ifuatayo (07828884555).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: