Ndani ya malalo tukufu: watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaliombea amani taifa la Iraq na raia wake.

Maoni katika picha
Hatuna mwingine zaidi yako ewe bwana unajua mazingira tuliyo nayo.

Uovu na dhulma vimezidi tunahitaji faraja.

Tuelekee kwa nani kila shia analia.

Haki imepotea duniani sharia imetoweka.

Iraq ipo katika dhima yako ewe mtoto wa mbora.

Raia wanahitaji kukuomba utupoze maumivu yetu.

Tumekuja kukushitakia machungu yetu utufute machozi.

Tunakuomba dua ewe Imamu wa zama.. tunakuomba ewe Imamu wa zama.

Kwa maneno hayo watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wakahitimisha dua yao, wanafanya hivyo kila siku ya Jumanne na Alkhamisi Alasiri wakiwa wamebeba bendera za Iraq, hawasahau kuombea taifa lao la Iraq, imekua kawaida yao kufanya hivyo toka kuanza kwa maandamano.

Baada ya kusoma ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuimba wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnu-Iba), walianza kuimba kaswida inayo eleza mazingira halisi ya taifa kwa sasa, wakimuomba Mwenyezi Mungu mtukufu na kutawasal kwa mtukufu wanaye mtumikia alipe taifa la Iraq na raia wake amani na utulivu na awaipushe na kila aina ya shari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: