Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa misaada katika uwanja wa uhuru huko Bagdad, inawapa waandamanaji misaada ya aina tofauti, kwa mara ya pili msafara wa kutoa misaada umekwenda kwenye uwanja wa uhuru na kupokelewa kwa furaha na waandamanaji. Msafara ulikua na kiwango kikubwa cha maji ya kunywa na vyakula vya aina mbalimbali, vitu hivyo vimesambazwa kwenye hema za Abulfadhil Abbasi (a.s) zilizofungwa eneo hilo.
Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilikua imesha tuma msafara mwingine kama huo siku za nyuma, katika mkakati wake wa kutoa misaada kwa waandamanaji na bado inaendelea kufanya hivyo katika mkoa wa Karbala.