Sauti ya raia: haya ndio yaliyosemwa na Marjaa Dini mkuu mwezi (19 Safar 1433h) sawa na (13 Januari 2012m).

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu alitahadharisha vyama vyote vya siasa toka zamani, kuhusu marumbano ya kisiasa yasiyo na tija kwa taifa, akavitaka vimalize tofauti zao na kutafuta ufumbuzi wa kulitoa taifa kwenye matatizo.

Tunajikumbusha yaliyo semwa na Marjaa Dini mkuu kwenye khutuba ya Ijumaa mwezi (19 Safar 1433h) sawa na (13 Januari 2012m), iliyotolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s), alisema kua mizozo ya kisiasa itakua na matokeo mabaya kwa taifa la Iraq siku za mbele, akatahadharisha vyama vya siasa kuendeleza mizozo na marumbano, akasema; vikao vya juu juu havitoshi kutatua tatizo, lazima kuwe na nia ya kweli ya kujadili kwa kina na kupata ufumbuzi wa kudumu sio kutuliza mambo tu.

Akaongeza: Inatakiwa vyama vya siasa visome mazingira ya nchi na viangalie mifumo ya siasa katika nchi zingine, sambamba na kuangalia migogoro ya kimataifa kwenye nchi zingine na kubaini mambo yanayo taka kufikiwa na nchi zingine, na athari yake kwa maslahi ya Iraq na mustakbali wake.

Mwisho akatahadharisha kuwa makini na watu wa nje, wasipewe nafasi ya kuingilia matatizo ya ndani ya Iraq, akasema: “Mitazamo ya watu wa nje haiwezi kutatua matatizo ya Iraq, watu wa nje wataangalia maslahi yao, na watafungua milango ya kuendelea kuingilia mambo ya ndani siku za mbele, hakuna ufumbuzi wa tatizo utakao fikiwa bila kuwepo na mazungumzo ya kweli yanayo fanywa na watu wanaohisi kuwajibika, viongozi lazima watafute njia ya kumaliza matatizo na kukidhi matakwa ya wananchi ya kuhakikisha taifa la Iraq linapata amani na utulivu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: