Idara ya ustawi wa jamii kupitia ofisi yake ya mkoa wa Dhiqaar inatoa misaada kwa waandamanaji.

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ofisi zake zilizo enea mikoani na mawakibu zinazo fungamana nayo, inaendelea kusaidia watu wanaofanya maandamano ya amani, ikiwemo ofisi ya mkoa wa Dhiqaar, imegawa mahitaji ya lazima kwa waandamanaji.

Misaada imegawanyika sehemu mbili kwa mujibu wa maelezo ya wasimamizi wa misaada hiyo: kwanza msafara wa kugawa misaada kwenye uwanja mkuu wa maandamano (uwanja wa uhuru) katika mji mkuu wa Bagdad, wamegawa vitu mbalimbali kama sehemu ya kuonyesha kuwaunga mkono hadi madai yao yatakapo fanyiwa kazi.

Sehemu ya pili ni kuendelea kutoa misaada kwa waandamanaji wa mkoani Dhiqaar kwenye uwanja wa Hububi, ambako zimejengwa hema maalum kwa ajili ya kutolea misaada ya chakula, matibabu nk..

Kumbuka kua idara ya ustawi wa jamii tangu kuanza kwa maandamano haya, imekua mstari wa mbele kusaidia waandamanaji katika uwanja wa uhuru Bagdad na mikoa mingine, wanatoa misaada ya aina mbalimbali kama vile:

  • - Kujenga heza za kutolea misaada.
  • - Kugawa chakula kwa waandamanji.
  • - Kugawa chaula kikavu, maji na juisi.
  • - Kutoa huduma za madibabu.
  • - Kuweka gari za wagonjwa katika maeneo ya waandamanaji.
  • - Msaada wa kimaanawiyya kwa kuwepo watumishi wa mawakibu kwenye viwanja vya maandamano.
  • - Kugawa baadhi ya vifaa vinavyo tumiwa na waandamanaji.
  • - Kufanya usafi katika maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: