Muhimu na hivi punde.. tamko la Marjaa Dini mkuu kuhusu hali inayo endelea Iraq.

Maoni katika picha
Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu amesoma tamko la Marjaa kutoka Najafu katika khutuba ya Ijumaa leo (2 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (29 Novemba 2019m), iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s).

Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi baada ya kusoma surat Fat-ha na kuwarehemu mashahidi watukufu amesema kua:

Mabwana na mabibi nakusomeeni tamko lililotufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani katika mji wa Najafu..

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema mwenye kurehemu

Marjaa Dini mkuu anafuatilia yanayo endelea kwa huzuni na masikitiko makubwa, hususan yaliyo tokea hivi karibuni katika mji wa Naswiriyya na Najafu, umwagaji mkubwa wa damu ulio tokea na uharibifu mkubwa wa mali na uchomaji moto wa majengo na uvunjaji.

Marjaa Dini mkuu anawarehemu mashahidi watukufu, na anazipa pole familia zao na kuwataka wawe na subira na uvumilivu, pia anawaombea majeruhi wapone haraka, kwa mara nyingine anasisitiza uharam wa kuwashambulia watu wanaofanya maandamano ya amani na kuwazuwia kudai haki zao, aidha anasisitiza uharam wa kushambulia mali za umma na binafsi pamoja na ulazima wa kutowaacha watu waovu wajipenyeze katika maandamano, ni jukumu la watu wanao andamana kwa amani kuwabaini watu wanaoleta vuruku na kufanya uharibifu na kuwafukuza, wasiruhusu watu hao kutumia maandamano ya amani kushambulia mali za umma na kushambulia watu.

Kutokana na mazingira magumu ambayo taifa linapitia kwa sasa, ukilinganisha na miezi miwili iliyo pita, bunge linatakiwa liangalie upya mambo haya, lifanye mambo yatakayo linda maslahi ya taifa na damu za wananchi, liangalie namna ya kumaliza vurugu na uharibifu, pia linatakiwa kuandaa haraka kanuni za uchaguzi huru na wa haki zitakazo ridhiwa na wananchi, kama sehemu ya utangulizi wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki, kuchelewesha jambo hili ambalo ndio msingi utakao saidia kututoa katika hali hii kwa amani chini ya muongozo wa katiba kutalighalimu sana taifa na kila mtu atajuta.

Maadui na vibaraka wao wanataka kufanikisha njama zao ovu za kusambaza fujo na vurugu na kuhakikisha wairaqi wanaingia katika mauwaji ya wao kwa wao, halafu walirudishe taifa katika zama za udikteka, lazima wananchi wote tushirikiane kuhakikisha hawafanikishi njama zao.

Hakima Marjaa Dini mkuu ataendelea kua ngome imara ya wananchi watukufu wa Iraq, jukumu lake ni kutoa nasaha na kuelekeza mambo yenye maslahi na wananchi, na wananchi wana haki ya kufanya jambo wanalo ona linafaida zaidi kwao wakati wa sasa na baadae.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: