Marjaa Dini mkuu awarehemu mashahidi wa maandamano na awaita kua ni watukufu pamoja na kuwaombea majeruhi wapone haraka.

Maoni katika picha
Katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (2 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (29 Novemba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, Marjaa Dini mkuu amewarehemu mashahidi wa vita ya islahi na kuzipa pole familia zao kutokana na msiba huo, hali kadhalika amesoma surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi kabla ya kuanza kusoma khutuba, na akawaombea wapone haraka majeruhi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Marjaa Dini mkuu anawarehemu mashahidi watukufu, na anazipa pole familia zao na kuwataka wawe na subira na uvumilivu, pia anawaombea majeruhi wapone haraka, kwa mara nyingine anasisitiza uharam wa kuwashambulia watu wanaofanya maandamano ya amani na kuwazuwia kudai haki zao, aidha anasisitiza uharam wa kushambulia mali za umma na binafsi pamoja na ulazima wa kutowaacha watu waovu wajipenyeze katika maandamano, ni jukumu la watu wanao andamana kwa amani kuwabaini watu wanaoleta vurugu na kufanya uharibifu na kuwafukuza, wasiruhusu watu hao kutumia maandamano ya amani kushambulia mali za umma na kushambulia watu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: