Marjaa Dini mkuu ametoa tahadhari kutokana na maadui wa Iraq pamoja na vibaraka wao wanaotaka kutimiza njama yao ya kueneza vurugu na uharibifu, kasisitiza kua lazima wananchi waungane kutibua njama hiyo.

Maoni katika picha
Katika khutuba ya Ijumaa leo (2 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (29 Novemba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, Marjaa Dini mkuu ametoa tahadhari kuhusu njama za maadui wa Iraq na vibaraka wao, wanaotaka kusambaza vurugu na uharibifu pamoja na kuhakikisha wananchi wa Iraq wanauwana wao kwa wao kwa kutumia maandamano yanayo endelea hivi sasa, ametoa wito kwa raia wa Iraq waungane kuvunja njama hiyo. Lifuatalo ni tamko kuhusu jambo hilo:

(Maadui na vibaraka wao wanataka kufanikisha njama zao ovu za kusambaza fujo na vurugu na kuhakikisha wairaqi wanaingia katika mauwaji ya wao kwa wao, halafu walirudishe taifa katika zama za udikteka, lazima wananchi wote tushirikiane kuhakikisha hawafanikishi njama zao).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: