Marjaa Dini mkuu alitaka bunge kuangalia upya mazingira ya taifa la Iraq kwa sasa yanayo tishia kuzama kwenye vurugu na uharibifu.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ametoa wito kwa bunge la Iraq liangalie upya mazingira ya taifa la Iraq kwa sasa, na lifanye maamuzi kwa kuangalia maslahi ya taifa, ili kuliokoa lisizame kwenye vurugu na uharibifu. Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (2 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (29 Novemba 2019m) ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ifuatayo ni sehemu ya kauli yake kuhusu swala hilo:

(Kutokana na mazingira magumu ambayo taifa linapitia kwa sasa, ukilinganisha na miezi miwili iliyo pita, bunge linatakiwa liangalie upya mambo haya, lifanye maamuzi yatakayo linda maslahi ya taifa na damu za wananchi, liangalie namna ya kumaliza vurugu na uharibifu, pia linatakiwa kuandaa haraka kanuni za uchaguzi huru na wa haki zitakazo ridhiwa na wananchi, kama sehemu ya utangulizi wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki, kuchelewesha jambo hili ambalo ndio msingi utakao saidia kututoa katika hali hii kwa amani chini ya muongozo wa katiba kutaligharimu taifa na kila mtu atajuta.)
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: