Marjaa Dini mkuu asisitiza kua yapasa kuwaacha raia wachague kilicho bara kwao bila kushurutishwa na yeyote.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza kua ataendelea kua pamoja ya raia wa Iraq, na kwamba nafasi yake ni kutoa nasaha na kuelekeza mambo anayo yaona yanamaslahi na wananchi, akasema kua yapasa kuwaacha wananchi wachague wenyewe wanacho kiona kina faida zaidi kwao bila kushurutishwa na yeyote.

Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (2 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na 29 Novemba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ifuatayo ni kauli yake katika jambo hilo:

(Hakima Marjaa Dini mkuu ataendelea kua ngome imara ya wananchi watukufu wa Iraq, jukumu lake ni kutoa nasaha na kuelekeza mambo yenye maslahi na wananchi, na raia wana haki ya kuchagua jambo wanalo ona linafaida zaidi kwao wakati wa sasa na baadae bila kushurutishwa na yeyote).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: