Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Tumegawa maelfu za sahani za chakula kwa waandamanaji na bado tunaendelea.

Maoni katika picha
Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kua tangu kuanza kwa maandamano ya amani, imesha gawa maelfu ya sahani za chakula kwa waandamanaji waliopo katika uwanja wa maandamano (uwanja wa Tarbiyya) mjini Karbala, na bado unaendelea kugawa chakula kila siku.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa mgahawa Mhandisi Aadil Hamami, akaongeza kua: “Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) unaendelea kugawa chakula kwa watu wanaofanya maandamano ya amani katikati ya mji wa Karbala, mamia ya sahani za chakula zinagawiwa kila siku kwa muda tofauti”.

Akabainisha kua: “Chakula hupikwa katika jiko la mgahawa na husafirishwa kwa gari maalumu hadi kwenye uwanja wa Tarbiyya ambao waandamanaji wameweka kambi, kiwango cha chakula kinaongezeka kutokana na kuongezeka kwa waandamanaji, wanagawa chakula moja kwa moja kutoka katika gari au katika mabanda ya Atabatu Abbasiyya yaliyopo hapo”.

Waandamanaji waliopo katika uwanja wa Tarbiyya wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa misaada yake kwao tangu kuanza kwa maandamano haya.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma mbalimbali kwa waandamanaji, miongoni mwa huduma huzo ni:

  • - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula, ambacho hupikwa katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kupelekwa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji safi ya kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai katika muda tofauti.
  • - Kutuma gari maalum za kusafisha maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji kwa waandamanaji.
  • - Kutoa huduma ya matibabu bure kwa waandamanaji na askari kupitia hospitali ya Alkafeel.
  • - Kujenga hema za kutolea mafunzo ya huduma ya kwanza na uwokozi kwa waandamanaji, sambamba na kutoa huduma ya uwokozi kwa waandamanaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: