Kituo cha turathi za Basra kinaangazia mafanikio ya watu wa mji huo.

Maoni katika picha
Mkoa wa Basra una utajiri mkubwa wa wanachuoni na watafiti wa fani mbalimbali, kwa ajili ya kuwatambulisha na kuangalia kazi zao, kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechukulia kua ni jukumu lake kufanya kazi hiyo kwa kutumia njia tofauti, miongoni mwa njia hizo ni uandishi wa kitabu cha kumbukumbu ya mambo ya kale ya Basra kiitwacho (Kandili za mitende.. kinacho elezea wasomi wa zamani wa Basra) juzu la kwanza, nacho kimeandikwa na Ustadh Muhammad Swalehe Abduridhwa.

Kitabu hicho kimeandika historia kwa ufupi za wanachuoni wa Basra, na kuangazia uzowefu wao kwa kutumia njia ya mahojiano, kituo kimefanya kazi kubwa sana kukamilisha kitabu hicho, kwani kimotokana na ukusanyaji wa nyaraka na Makala zilizo kua zimesambaa sehemu mbalimbali, sambamba na kutafuta picha zinazo endana na wahusika, kisha ukafanyika uhakiki wa lugha.

Kumbuka kua kituo cha turathi za Basra kinaendelea kuandika vitabu na majarida kuhusu turathi za mji wa Basra, kwa ajili ya kutoa mchango wake katika maktaba za kiarabu na kiislamu, na kuangazia nafasi ya mji huu katika sekta tofauti za elimu.

Kuangalia kitabu hicho na vitabu vingine vilivyo andikwa na kituo hiki, tembelea sehemu ya maonyesho ya vitabu yaliyopo karibu na mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) au fungua toghuti ifuatayo: http://www.mk.iq/releases.php
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: