Mazuwaru wanamuomba Mwenyezi Mungu alipatie amani taifa la Iraq mbele ya Maqaam ya muokozi wa umma Imamu wa zama (a.f).

Maoni katika picha
Mbele ya Maqaam takatifu ya Imamu wa zama (a.f), idara ya ofisi ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeratibu kikao cha kuliombea amani taifa la Iraq na watu wake, na wamewatakia rehema mashahidi na uponaji haraka wa majeruhi, washiriki wa ratiba hiyo walikua ni watumishi wa ofisi ya wanawake na mazuwaru wa kike.

Kikao hicho cha dua ni sehemu ya kuonyesha kuunga mkono maandamano ya amani yanayo endelea, ndipo wakamuomba Mwenyezi Mungu alilinde taifa la Iraq na raia wake pamoja na Marjaiyya takatifu kwa utukufu wa Imamu wa zama (a.f).

Akaongeza kua jambo hili ni sehemu ya kuhuisha utiifu kwa Imamu wa zama na kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, anayetaka kuzuwia kuingiliwa na watu wa nje na umuhimu wa kubadilisha kanuni za uchaguzi na kuacha ufisadi uliojaa katika taasisi za serikali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: