Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Hindiyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya inatoa mafunzo ya kusoma adhana na misingi yake.
Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa tawi hilo Sayyid Haamid Marábi amesema: “Ni Imani ya Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya na matawi yake ya kuipatia jamii waadhini wenye uwezo na sauti nzuri zinazo burutisha nyoyo za waumini, washiriki wa semina hii ni maustadhi wa Maahadi na wanafunzi wao pamoja na watu wengine”.
Akaongeza kua: “Mkufunzi wa semina hiyo ni Ustadh wa usomaji na msimamizi mkuu wa malezi Twalibu Ifaari, amefundisha mada nyingi, kubwa ikiwa ni adhana na aina zake pamoja na mambo ya lazima katika adhana kilugha, sambamba na naghma na misingi ya usomaji wa adhana”.
Tambua kua Maahadi ya Quráni tukufu hufanya semina za masomo tofauti kwa ajili ya kuunda kizazi cha wasomi wa Quráni wanao shikamana na mafundisho yake matukufu, aidha hufanya vikao na mahafali za usomaji wa Quráni kupitia matawi yake ya mikoani.