Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zatangaza kufanya majlisi ya kuomboleza watu waliokufa kwenye maandamano ya Iraq.

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya Jumapili ya leo (4 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (1 Desemba 2019m), umetangaza kufanya majlisi ya kuomboleza watu waliopata shahada (walikufa) kwenye maandamano ya Dhiqaar na Najafa pamoja na mikoa mingine ya Iraq, walio uwawa kwenye matukio ya kusikitisha ya hivi karibuni.

Majlisi itafanywa katika eleo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kesho Jumatatu kuanzia saa nane Adhuhuri hadi saa kumi na moja jioni.

Majlisi hii inaonyesha kushikamana na familia za mashahidi na kuwapa pole kwa msiba huu, na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awape subira na uvumilivu pamoja na kulilinda na shari taifa la Iraq na raia wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: