Majeruhi wa maandamano ya Dhiqaar: Hospitali ya Alkafeel imetuma kikosi cha madaktari na dawa pamoja na vifaa tiba.

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma msafara wa misaada ya kitabibu pamoja na kikosi cha madaktari, kwa ajili ya kwenda kuwatibu watu waliojeruhiwa kwenye maandamano ya Dhiqaar na kulazwa kwenye hospitali ya Hussein (a.s) katika mkoa huo.

Msaada huu ni sehemu ya misaada mingi ya kibinaadamu inayo tolewa na hospitali ya Alkafeel, pia ni muendelezo wa huduma wanazo pewa watu wanaojeruhiwa kwenye maandamano tangu siku ya kwanza, chini ya program ya (matibabu bila malipo).

Uongozi wa hospitali umesema kua: “Kutokana na hali iliyopo katika hospitali tumeamua kutuma kikosi cha madaktari kwenda kusaidia kuwatibu watu waliojeruhiwa kwenye maandamano mkoani Dhiqaar na wale watakao kuwa na hali mbaya wataletwa katika hospitali ya rufaa Alkafeel kwa matibabu zaidi”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma za aina mbalimbali kwa waandamanaji, miongoni mwa huduma hizo ni:

  • - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula kinacho pikwa katika mgawaha wa Atabatu Abbasiyya na kutumwa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji ya kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa wakati tofauti.
  • - Kufanya usafi katika sehemu zinazo tumiwa na waandamanaji kwa kutumia kari maalum za usafi.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji kwa waandamanaji.
  • - Kutoa huduma za matibabu bure kwa kila mtu anayepata matatizo ya afya kwenye maandamano raia au askari.
  • - Kujenga hema za kufundisha huduma ya kwanza na uwokozi kwa waandamanaji sambamba na kutoa huduma za uwokozi.
  • - Kutima misafara ya kutoa misaada kwa waandamanaji katika uwanja wa uhuru mjini Bagdad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: