Kikosi cha madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa kushirikiana na madaktari wa hospitali ya Hussein (a.s) katika mkoa wa Dhiqaar kimeanza kuwafanyia vipimo mbalimbali watu waliojeruhiwa kwenye maandamano ya amani.
Zowezi la upimaji linaenda sambamba na kubaini wagonjwa watakao hamishiwa hospitali ya rufaa Alkafeel, kwa kutumia gari zake za wagonjwa.
Pamoja na kutoa huduma ya upimaji kikosi hicho pia kimetoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa.
Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel imetuma msafara wa dawa na vifaa tiba pamoja na kikosi cha madaktari kwa ajili ya kuwatibu watu waliojeruhiwa kwenye maandamano mkowani Dhiqaar hivi karibuni, na kulazwa kwenye hospitali ya Hussein (a.s).