Majlisi ya kuomboleza: Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zinafanya majlisi ya kuwarehemu mashahidi wa maandamano ya Iraq.

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya unaomboleza mashahidi wa vita ya islahi, miongoni mwa watu wanaofanya maandamano ya amani ya kudai haki zao walizopewa kikatiba na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu, yamefanywa baada ya Adhuhuri ya leo (5 Rabiu-Aakhar 1441h) sawa na (2 Desemba 2019m), hususan mashahidi wa Dhiqaar, Najafu, Bagdad na Karbala.

Majlisi hiyo imefanywa katika moja ya sehemu zilizo pauliwa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, na kuhudhuriwa na makatibu wakuu wa Ataba mbili tukufu pamoja na watumishi wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na idadi kubwa ya mazuwaru waliokuwepo eneo hilo.

Rais wa kitendo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Swalahu Karbalai ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kikao hiki ni sehemu ya kuonyesha kushikamana na watu wa Dhiqaar pamoja na familia za mashahidi na kuwapa pole kutokana na msiba huu, sambamba na kuunga mkono maandamano ya amani ya kudai mabadiliko na maisha bora, na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awape subira na uvumilivu, pamoja na kulilinda taifa la Iraq na raia wake kutokana na kila aina ya shari”.

Naye rais wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili Ustadh Naafii Mussawi akasema kua: “Uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya umezowea kuwakumbuka mashahidi wa taifa kwa kufanya harakati mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya kuomboleza na kuwapa pole familia za mashahidi”.

Kumbuka kua siku za hivi karibuni vimeshuhudiwa vifo kadhaa vya waandamanaji na idadi kubwa ya majeruhi katika kadhaa, huku mkoa wa Dhiqaar na Najafu ikiwa na waathirika wengi zaidi ukilinganisha na mikoa mingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: