Atabatu Abbasiyya tukufu yatuma msafara wa misaada kwa waandamanaji walioweka kambi kwenye uwanja wa uhuru jijini Bagdad.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma msafara mwingine wa misaada kwenye uwanja wa uhuru jijini Bagdad, kama sehemu ya kuunga mkono maandamano ya amani yanayo ruhusiwa na katiba ya Iraq na kuungwa mkono na Marjaa mtukufu, maandamano ya kudai islahi na maisha bora.

Huu ni msafara wa tatu, umesheheni maji ya kunywa kwa wingi na vyakula pamoja na mambo mengine, wamegawa vitu hivyo kwenye mahema yaliyopo uwanjani hapo, makao makuu ya maandamano ya Bagdad, sehemu ambayo imekua na waandamanaji tangu tarehe 25 Oktoba hadi leo.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu tangu yalipo anza maandamano ya Iraq imekua ikitoa misaada mbalimbali kwa waandamanaji katika mji wa Karbala na Bagdad, hivi karibuni hospitali ya Alkafeel ambayo iko chini yake imetuma kikosi cha madaktari na dawa pamoja na vifaa tiba kwenda kusaidia watu waliojeruhiwa kwenye maandamano ya amani katika mkoa wa Dhiqaar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: